CHAMA CHA WANYWAJI
Nimeanzisha chama changu,
Nani anataka kujiunga?????
Itabidi tujaze kwanza fomu za kugombea
urais, nimeshamuhonga msajili wa vyama na mwenyekiti
wa tume ya uchaguzi kwa hiyo ingawa tumechelewa
hatutapata shida.
kabla ya sera tunaanza na majukumu, hebu kwanza pata
undani.......................................
ZIFUATAZO NI ADHABU ZITOLEWAZO KWA UVUNJAJI WA SHERIA
ZA CHAMA CHA WANYWAJI
1. Kosa la kumtoroka mlevi mwenzako kwenye bar - Jela
miezi tisa
2. Kuacha kunywa pombe na fedha unazo - Kifungo cha
maisha
3. Kuvunja chupa ya beer - Jela miaka miwili
4. Kumkaribisha mume au mke wa rafiki yako bila idhini
yake - Viboko ishirini vya makalio na kufungiwa kunywa
nusu siku
5. Kuomba kununuliwa chakula au kununua chakula au
bidhaa kwa wamachinga wakati wa kukata maji, na ukijua
dhahiri pesa ya pombe inapungua - Jela miezi tisa
6. Kumchukulia dhamana mtu asiyepiga (mma) pombe
adhabu yake ni - kutolewa kwenye chama
7. Kumwibia pombe mlevi mwenzako ni kosa kubwa - Jela
mwaka mmoja
8. Kukataa kunywa wakati umekaribishwa - Jela miaka
mitano
9. Kukwepa ulevi wa aina yoyote adhabu - kunyang'anywa
mke au mume kama huna utaozwa/kuozeshwa mke au mume
kwa nguvu
10. Kupita Bar au Grocery na kujifanya huoni hilo ni
kosa kubwa faini yake ni -kuwanunulia wanywaji wote
waliokuwa kwenye Bar/Grocery kila mtu kinywaji
anachokunywa na kukaa ukiwaangalia hadi wamalize
11. Kumcheka mnywaji mwenzako akiwa amelewa ni kosa la
jinai, unachotakiwa kufanya ni kumpongeza kwa kazi
nzito aliyofanya, adhabu yake ni - Kutolewa kwenye Bar
muda wa dakika moja
12. Kumshawishi mlevi kuacha pombe kwa kisingizio eti
ajenge nyumba au asomeshe watoto - Kunyongewa Bar
13. Kukataa kunywa kwa madai unajenga adhabu ni -
kuwanunulia bia wenzako hadi utakapomaliza ujenzi
14. Ukinywa pombe halafu utapike adhabu ni - Kurudia
kunywa hadi ulewe tena
Wenu mshiriki
No comments:
Post a Comment